"Mimi mwenyewe sikusikia interview ya mama yangu, nilisikia tu ameongea lakini sikujua ameongea hivyo kwa madhumuni gani lakini mi sipendi sana vitu vyangu na familia yangu kuviweka wazi, nadhani ni matatizo tu ya ndani ya familia, sisi wenyewe na mapenzi yetu ndo imefanya ifikie mwisho na Mwenyezi Mungu pia amependa iwe mwisho wetu, kwa hiyo hatuna jinsi.
Petit Man amesema kwa sasa yeye na mkewe Bi Esma ambaye wamezaa mtoto mmoja wanaishi sehemu tofauti, huku kila mmoja akiendelea na maisha yake binafsi.
"Mimi siko tena nae nishaachana naye, ye anaishi kwake na mimi naishi nyumbani kwangu, ninaposema mtu nimeachana nae nimemaanisha, nimetoa talaka tatu yani siko nae tena yani", alisema Petit Man.
EmoticonEmoticon