Saturday, 26 March 2016

“Johan Cruyff ni kama baba yangu” – Guardiola 0

Siku mbili baada ya kutoka kwa taarifa ya kifo cha nguli wa soka wa Uholanzi na Barcelona, Johan Cruyff ambaye chanzo cha kifo chake kinatajwa kuwa ugonjwa wa Saratani, Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola amemtaja nguli huyo kama mtu muhimu katika maisha yake akimlinganisha na baba yake.
Akizungumza na kituo cha Rac-1 cha Catalan, Hispania, Guardiola alisema amemfahamu Cruyff kama mtu muhimu katika maisha yake ya soka na kuwa mtu ambaye alimsaidia kujua soka ni nini.
“Nilikuwa sijui kitu kwenye soka kabla sijakutana na Cruyff … Johan Cruyff alikuwa kama baba yangu kwa mambo ambayo alikuwa ananifanyia,
“Katika soka baada ya kumaliza kucheza soka na kuamua kuwa kocha sababu tu unataka kufundisha, unaweza kufikiri utakuwa kama vile unavyofikiri lakini mambo ni magumu mpaka unapokuwa na majina kama ya kina Messi na Johan alitusaidia kufanya hivyo,” alisema Guardiola ambaye msimu ujao atahamia Manchester City.


EmoticonEmoticon

 

Video of the day